KAGERE ASIMULIA ALIVYOMUOTA KAKOLANYA
Meddie Kagere amesema haikuwa bahati yake kuwafunga Yanga huku akisisitiza kwamba Beno Kakolanya ni kipa.
Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na matokeo kumalizika kwa suluhu, Kakolanya ndiye aliibuka shujaa kutokana na umahiri wake wa kuokoa hatari zilizokuwa zikielekea golini kwao.
Kagere ambaye mashabiki wa Simba walikuwa wakimwaminia kwamba atakinukisha, ni kati ya wachezaji waliokosa nafasi za wazi katika mchezo huo uliojaa upinzani mkubwa baada ya shuti lake alilolipiga ndani ya 18 kupaa huku mashabiki wakiamini kuna mkono wa mtu.
Kagere alisema kipa huyo alijitahidi kumsoma yeye na washambuliaji wenzake Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya ambao wote walipata nafasi za kufunga na kushindwa kuzitumia vema.
“Tulicheza vizuri lakini hatukuwa na bahati ya ushindi katika mchezo huo na hilo lipo wazi kabisa kwa kila shabiki aliyejitokeza uwanjani kuangalia mchezo huo.
Post a Comment
0 Comments