LIGI KUU VPL
Uchawi wawaibua Coastal Union
labu
ya Coastal Union imeibuka na kuzungumzia kuhusu tetesi za mchezo wa
ligi kuu Tanzania bara kati ya watani wa jadi Simba na Yanga kuhusishwa
na masuala la kishirikina.
Mchezo
huo ambao ulipigwa wikiendi iliyopita katika uwanja wa taifa,
ulimalizika kwa sare ya bila kufungana huku ikishuhudiwa Simba ambayo
ilikuwa mwenyeji wa mchezo huo ikikosa nafasi nyingi za kufunga, jambo
ambalo mashabiki wake wamelihusisha na masuala ya kishirikina.
Akizungumza na www.eatv.tv kwa upande wa klabu yake kuhusiana na suala hilo, Afisa Habari wa Coastal Union, Hafidh Kido amesema,
" Kwanza niwathibitishie kabisa watu kuwa uchawi katika mpira haupo na kama upo basi watu wanapoteza pesa zao bure kwa waganga lakini uchawi pekee ambao unatumia katika soka ni nidhamu pamoja na mazoezi ya nguvu ".
" Kitu kikubwa sana kilichotufanya sisi Coastal Union kuwa vizuri ni hasira kwasababu sisi ni moja ya klabu kubwa kabisa nchini ukiondoa Simba na Yanga lakini tuliona kuwa hatutajwi ndio maana wachezaji wamekuwa na hasira ya kutaka kufanya vizuri katika kila mchezo ", ameongeza.
Coastal Union inakamata nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu kwa alama zake 13 baada ya kushuka dimbani michezo nane.
Kati ya klabu nne zilizopanda ligi msimu huu, Coastal Union na JKT Tanzania pekee ndizo klabu zilizo katika nafasi ya juu katika ligi tofauti na klabu zingine nne zilizobakia.

Post a Comment
0 Comments