Wachezaji wawili Yanga waongeza nguvu



Wachezaji wawili wa Yanga Baruan Akilimali na Juma Abdul wamerejea kikosini leo, Baada ya kuugua kwa muda mrefu. 

Wachezaji hao walikuwa wanasumbuliwa na majeraha na kupelekea kukosekana ndani ya dimba kwa miezi kadhaa. 

Abdul na Akilimali wameanza mazoezi leo kuelekea mechi ijayo ya ligi kuu dhidi ya Mbao FC itakayopigwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Yanga itamenyana na Mbao kwa mara ya kwanza msimu huu ambayo ilitoka kuiadhibu Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza hivi karibuni. 

Post a Comment

0 Comments