Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 Iiliyokua ikisafiri kwenda NAIROBI imeanguka

Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.
Ofisi ya waziri Mkuu wa Ethiopia, Abey Ahmed imetoa taarifa ikitoa rambirambi kwa familia za walio wapoteza wapendwa wao katika jali hiyo.
Kampuni hiyo ya ndege imesema kuwa taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitatolewa muda sio mrefu
source: DAR24

Post a Comment

1 Comments

  1. imeanguka muda mfupi baada ya kuruka ikiwa na watu 157.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika hilo la ndege, ndege hiyo yenye nambari ET 302, ilipoteza mawasiliano ikiwa katika anga la jiji la Addis Ababa baada ya kuanza safari yake majira ya saa mbili asubuhi kwa saa za ukanda wa eneo hilo ikitokea katika Uwanja wa Kimataifa wa Bole.

    Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na eneo la Bishoftu, Kusini Mashariki mwa Addis Ababa.

    “Hadi sasa zoezi la utafutaji na uokoaji linaendelea na hatujapata taarifa zozote zilizothibitishwa kuhusu watu walionusurika au hata majeruhi,” imeeleza taarifa ya Ethiopian Airlines.

    “Timu ya wafanyakazi wetu itatumwa kwenye eneo la ajali kwa ajili ya kutoa msaada wowote kadiri wawezavyo,” imeongeza.

    Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ametumia mtandao wa Twitter kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

    ReplyDelete