MUENDELEZO WA HISTORIA YA Sir Jayantilal Keshavji Chandy (Sir Andy) - 1928 - 2017 SEHEMU 3

Sir Jayantilal Keshavji Chandy (Sir Andy) - 1928 - 2017






CHAPTER 3:FAMILY BUSINESS:



Sir Andy Chande alirudi Tanganyika akiwa amejipanga akilini kujiunga na biashara za familia ambazo kwa wakati huo zilikua zimetanuka sana.kampuni za kina Chande wakati huo zilikua ndio muuzaji nje(exporter)mkubwa wa kahawa nchini Tanganyika,pia walikua wanasafirisha alizeti,asali,nta na pamba kwenda Ulaya.

Tofauti na matarajio yake alipofika Sir Andy Chande hapa DSM akaambiwa hawezi tu kujiunga na biashara hapa mjini na kua boss,lazima aende kijijini kule kuanza kufanya kazi kule ndio ajifunze biashara vizuri kuanzia chini kabisa na ndio aje juu(wabongo tunaweza hii?mtoto wa boss aje kwenye kampuni halafu aanzie chini kabisa kijijini!).

Alihuzunika sana Ila hakua na jinsi na ikamlazimu arudi Bukene Tabora kuanza kujifunza biashara kwa baba yake mdogo!.alipofika kule alianza kazi mara moja,huku wakianza kazi kuanzia 12 asubuhi mpaka 7:30 usiku kila siku.baada ya kufanya kazi kwa wiki 14 ndio akaambiwa ameiva anaweza kwenda Dar sasa kujifunza zaidi.

Alipofika Dar nako hakufika kua boss,badala yake aliwekwa kwenye kazi ndogo ndogo za ofisini kama kufuatilia barua,kuandaa bili etc.huku baba yake mdogo mwingine na baba yake wakimsamia kwa karibu kwenye biashara yao ya exports. Sir Andy Chande anasema taratibu alianza kujifunza na kuijua biashara vizuri.

Anasema lakini tofauti na baba yake ambae alikua mtu wa dini na sio wa kujichanganya sana,yeye alipenda kujichanganya na watu mbalimbali na ilimfanya ajulikane sana Dar.

Baadae alijiunga na kikundi cha mambo ya utamaduni ambacho kilikua hakibagui rangi watu wote wazungu na weusi walikuwemo na ilimpa fursa nzuri ya kujenga marafiki wa aina zote.japo baba yake alimuonya asijiingize kwenye siasa.

Baadae anasema baba yake na ndugu zake waligombana kwenye biashara zao na wakagawana mali.nduguze wa baba yake waliuza biashara zao na kurudi India na baba yake alibaki Tanganyika na akamteua yeye Chande kua mtendaji mkuu wa makampuni yao na haswa akisimamia kiwanda cha usagaji cha Pugu road(sasa hivi cha Bakheressa pale Tazara).

Anasema hapo ndipo akawajua wafanyabiashara mashuhuri wa kizawa wakiwema Dossa Aziz na John Rupia ambao walikua wanawauzia mpunga.

Sir Andy Chande aliendelea na maisha yake ya kijamii huku akiteuliwa kua kwenye bodi ya ukaguzi wa filamu kazi ambayo anasema alikua akitegea sana,kwani akienda cinema movie ikianza tu anatoroka na anarudi kimyakimya ikikaribia kuisha kwani anasema movie za kihindi zilikua ndefu sana zinamchosha!.

Pia aliteuliwa kua mmoja kati ya watu wa jumuiya ya wafanyabiashara iliyoitwa ceoroundtable ambayo ilianza miaka ya 1920 na sasa ilikua Afrika,yeye alikua mtu wa kwanza ambae sio mzungu kuteuliwa(kwasasa kwenye hii jumuiya wapo kina Ali Mufuruki).

Baadae baba yake aliugua na kansa na wakaazimia kumpeleka marekani kutibiwa lakini mzee alipofika Nairobi,akageuza akisema anajua hawezi pona bora arudi atumie muda mchache uliobakia na familia yake.mnamo mwezi August mwaka 1959 baba mzazi wa Sir Andy Chande alifariki dunia!.

itaendelea...

Post a Comment

0 Comments