MICHEZO KIMATAIFA
AL HILAL, MABILIONEA WA SUDAN WALIOMUAJIRI ULIMWENGU, ACHANA NA UWANJA WANAMILIKI HOTELI YA KISASA
NA SALEH ALLY, KHARTOUM
NENO
Al Hilal maana yake ni mwezi, hili ni jina la timu nyingi sana duniani
hasa zile zinazotokea katika nchi mbalimbali za Kiarabu au zenye asili
hiyo.
Licha
ya rundo la timu zinazotumia jina hilo, Al Hilal Omdurman ya Sudan
ndiyo timu ya kwanza kuanza kuitwa jina hilo mwaka 1930, sasa ni miaka
88 iliyopita.
Klabu
hiyo ni maarufu zaidi nchini hapa na inashindana na wapinzani wao
wakubwa El Merreikh ambao pia ni maarufu na moja ya timu tajiri barani
Afrika.
Omdurman
ni eneo linalojitegemea likiwa ni upande wa pili wa Khartoum baada ya
kuvuka Mto Nile. Ndiyo maana klabu hiyo ikapewa jina la Al Hilal kutoka
Omdurman ambako pia wanatokea wapinzani wake, El Merreikh na viwanja vya
klabu hiyo mbili, viko jirani kabisa.
Al
Hilal inamiliki uwanja unaojulikana kwa jina la Al Hilal Stadium,
uwanja huu unakadiriwa kufikisha hadi watu 65,000 wanaoingia lakini
kitaalamu kwa uwanja ambao una viti na watu kuingia kwa nafasi, angalau
watu 40,000.
Klabu ya Al Hilal inatajwa kuwa moja ya klabu tajiri barani Afrika na Mtanzania, Thomas Ulimwengu anaitumikia kupitia timu yake.
Timu
inayomilikiwa na klabu hiyo ndiyo inayoongoza kwa mashabiki hapa Sudan
na ukubwa wake unaifanya iwe gumzo zaidi kuliko nyingine zote.
Mashabiki
wa Al Hilal ni wale wenye wazimu hasa wa soka ambao wanapokasirika huwa
ni hatari sana kwa kuwa wana uamuzi mgumu na wanaweza kudhuru wakati
wowote.
Wakati wa mechi za Al Hilal kumekuwa na ulinzi mkali hasa inapocheza na timu ambazo zinaaminika zina upinzani mkali dhidi yake.
Kikundi
chake cha ushangiliaji cha Al Hilal Utras, ndicho kinaaminika kuwa na
mashabiki watukutu zaidi barani Afrika kikifananishwa na kile cha Al
Ahly ya Misri au Club African ya Tunisia kwa kuwa wao kuumiza si jambo
gumu kwao na wamekuwa wakipambana na askari inapoonekana wamekerwa.
Mwenyekiti
wake ni bilionea Ashraf Seed Ahmed, mmoja wa watu maarufu nchini hapa
na hivi karibuni alikubali Thomas aongezwe katika kikosi chake bila ya
kujali hakuwa amepona sawasawa.
Ulimwengu
alisajiliwa na Ah Hilal huku mwenyekiti huyo akiunga mkono kwa kuwa
tayari alishamuona Ulimwengu akiitumikia TP Mazembe ya DR Congo na
kufanya vizuri.
Wakati
Ulimwengu ametua kwa takribani miezi miwili, Al Hilal ilimuajiri kocha
wake wa zamani Lamine N’Diaye raia wa Senegal ambaye alifanya naye kazi
wote wakiwa TP Mazembe na kufanya vizuri.
Kwa
hadithi, unaweza kuamini Ulimwengu amepotea kwenda Sudan lakini kama
utazungumza suala la mafanikio kwa kuangalia yuko, Ulimwengu ambaye
alikaa nje na kushindwa kucheza kwa takribani miezi sita kutokana na
kuandamwa na majeraha, unaweza kusema ni mchezaji mwenye bahati.
Wachezaji
wengi ambao wako fiti na wanategemewa na klabu zao, wangetamani kupata
nafasi ya kucheza Al Hilal lakini inashindikana licha ya juhudi za dhati
kwa na hata mawakala wao.
Ulimwengu alikubalika tangu akiwa bado mgonjwa, jambo ambalo lilikuwa ni kuonyesha imani ya kiwango cha juu sana.
Klabu hiyo imezaliwa mwaka 1930, miaka mitano baadaye ikazaliwa Yanga na ulipoongezeka mmoja na kuwa sita, ikazaliwa Simba.
Pamoja na kupishana miaka mitano na sita, utakapoamua kuzifananisha, utakuwa unazungumzia mfano tofauti sawa na mbingu na ardhi.
Uwanja
mkubwa kama wa Al Hilal, si jambo dogo tena ni uwanja ambao ndani yake
kuna hoteli kubwa ya kisasa ambayo wachezaji huweka kambi.
Hoteli
hiyo iko ndani ya uzio wa Al Hilal Stadium na ina vyumba takribani 50
vya kisasa kabisa na ina sehemu tatu za kupumzikia zikiwa na makochi ya
kisasa na mapokezi pia.
Upande
huo wa mapokezi unaambatana na sehemu ya chini ya kupumzikia lakini
kuna sehemu nyingine juu na zote zinatumika kwa ajili ya wageni wachache
maalum wa klabu hiyo lakini hasa ni mahsusi kwa ajili ya wachezaji
wanapoweka kambi.
Wachezaji
wa Al Hilal wanapokuwa kambini angalau kwa siku mbili, wanaweka kambi
katika hoteli hiyo ya kisasa ambayo mbele yake kuna sehemu maalum ya
kupumzikia yenye majani.
Al
Hilal ni kati ya klabu chache kabisa za Ukanda wa Afrika Mashariki
zinazojitambua. Maana inamiliki redio yake, runinga yake na pia gazeti
lake. Hivyo ina timu kubwa ya vyombo vya habari.
Vyombo
hivyo vya habari vimekuwa vikifanya kazi ya kuitangaza na kuisaidia Al
Hilal kuongeza mashabiki na kwa ushirikiano mkubwa na vyombo vingine vya
habari.
Tofauti
na nyumbani, timu hata ikianzisha gazeti tu, tayari inatengeneza uadui
na vyombo vingine vya Tanzania kama vile kuvikomoa na kadhalika. Al
Hilal imekuwa ikisisitiza suala la umoja na vyombo vya habari hauwezi
kuvunjwa.
Meneja
wa Al Hilal, Mohamed Haroun amezungumza na na blog yako pendwa ya
SALEHJEMBE katika eneo la Omdurman na kusisitiza kwamba wanajitambua na
kikubwa kwao ni ndoto ya ubingwa Afrika.
“Tunataka kuwa mabingwa, tumelikosa kombe mara zote lakini tunataka kuwa mabingwa wa Afrika ili kutimiza ndoto zetu,” anasema.
“Tunajua
tuna mafanikio makubwa katika suala la biashara na uendeshaji, lakini
kuitwa mabingwa wa Afrika ni jambo tunalolipa kipaumbele kweli,”
anasisitiza.
Ukiachana na meneja huyo, Ulimwengu yeye anasema alipajua Sudan kabla hajatua Al Hilal.
“Nilikuja
hapa mara mbili na TP Mazembe. Mara moja nilifunga dhidi yao na wakati
mwingine dhidi ya Merreikh. Hivyo walikuwa wakinijua vizuri, hii
ilinisaidia hata kuzoea hapa mapema,” anasema.
“Kwa
maana ya klabu kweli mambo yanafuata weledi, utaratibu sahihi na kila
kitu kimepangwa. Hii ni klabu kubwa sana tofauti na wengi
wanavyofikiria. Huenda kwa kuwa iko Sudan, wengi kuichukulia poa.
“Kwa
maisha hapa, kila mtu ana yake. Pia watu wanapenda sana mpira hivyo
kuheshimika kama unafanya vizuri ni jambo la sekunde tu.”
Al
Hilal inamiliki uwanja huo mkubwa, inamiliki mali nyingi hadi hoteli na
hapa ndiyo unagundua ukubwa wake huku ikiwa moja ya timu inayoheshimika
sana kisoka barani Afrika ingawa bado hawajatimiza ndoto ya kuwa mabingwa wa Afrika.
Ulimwengu
ameamua kutua Sudan na kufanya kazi na sasa kwa wale waliokuwa hawajui
au waliona amekosea, wanaweza kuelewa kuhusiana na Al Hilal.
Kama
hiyo haitoshi, Jumatano tutakuletea kugusiana na namna Ulimwengu
ambavyo amekuwa gumzo katika soka la Sudan lakini anavyoishi kwa kukwepa
usumbufu wa mashabiki barabarani au kila anapotembea.
Post a Comment
0 Comments