MICHEZO
DREAMLINER YA AIR TANZANIA KUIPELEKA TANZANIA CAPE VERDE, MASHABIKI WAITWA WAJITOKE
Timu
ya Taifa Stars, itasafiri na ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner kwenda
nchini Cape Verde kuwavaa wenyeji wao katika mechi ya kuwania kufuzu
Afcon 2019 nchini Afcon.
Ndege
hiyo itaruka kwa saa 9 bila kutua hadi nchini humo. Mashabiki
wametakiwa kujitokeza kukata tiketi kwa ajili ya kwenda kuishangilia
Stars. Kikosi hicho na mashabiki wake watarejea siku hiyohiyo baada tu
ya mechi.
Tayari Taifa Stars imeanza maandalizi ya mchezo huo chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria.
Baada
ya mechi hiyo, Stars itarejea nchini mara moja kuja kujiandaa na mechi
ya marudiano dhidi ya Cape Verde jijini Dar es Salaam.
Post a Comment
0 Comments