Mabosi Yanga wapewa sharti hili na Zahera


Licha ya kuondoka nchini kuelekea kwao Congo kwa majukumu ya kukinoa kikosi cha taifa lake kama Msaidizi, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewataka mabosi wake kuhakikisha wanamuongezea mkataba mpya, kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu.

Zahera amewataka waajiri wake kufanya hivyo haraka kwa maana mkataba wake unaelekea ukingoni ili wasije wakamkosa hapo baadaye.

Kocha huyo ameamua kuliibua hilo mapema ili kuendelea kumtumia mchezaji huyo ambaye amekuwa na mchango muhimu pia sehemu ya wachezaji tegemeo ndani ya kikosi cha Yanga.

Ajibu ambaye alijiunga na Yanga baada ya msimu wa 2016/17 kumalizika akitokea Simba, alisaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa kihistoria ambao kwa sasa unaelekea ukingoni.

Mpaka sasa Ajibu ameisaidia Yanga kutengeneza jumla ya nafasi 4 za kufunga tangu msimu huu uanze na akipasia kambani bao moja.

Post a Comment

0 Comments