MBELGIJI AWAPIGA 'STOP' WATANO SIMBA


Mratibu wa Simba, Abbas Ally ameweka wazi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems aliwazuia nyota wake wa kimataifa walioitwa timu za taifa.

Maamuzi hayo yalikuja kutokana na kuwapa maandalizi ya kucheza na African Lyon ambayo jana walifanikiwa kuiadhibu kwa mabao 2-1.

“Hadi sasa hakuna hata mchezaji wetu wa kimataifa aliyeondoka, kutokana na kupata taarifa mapema juu ya uwepo wa mchezo wetu wa kesho (jana) dhidi ya African Lyon.

“Kweli baada ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Yanga, kocha aliahidi kuwaruhusu waende kutumikia timu zao za taifa kwani alitegemea ligi ingesimama kupitisha kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars, lakini baadaye aliwazuia baada ya kutan­gazwa kutosimama kwa ligi hivyo akawataka wabaki hadi wamalize mechi ya kesho (jana),” alisema Abbas.

Wachezaji wanaotakiwa kujiunga na timu zao za taifa ni Meddie Kagere na Haruna Niyonzima wote raia wa Rwanda, Juuko Murshid na Emmanuel Okwi wote Uganda huku Clatous Chama akiitwa Zambia.

Post a Comment

0 Comments