YANGA WATOA KAULI YA KUTISHA
Wakati kikosi cha Yanga kikiwa tayari kushuka dimbani leo kuwakabili Mbao FC ya Mwanza, uongozi wa timu hiyo umesema kuwa watawaonesha kuwa wao si Simba.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema licha ya Mbao kuwa wazuri msimu huu hata wao wapo vizuri.
Ten ameeleza katika mechi zote walizocheza hawajapoteza hata mmoja na badala yake walienda suluhu tasa dhidi ya Simba Septemba 30.
Timu zote mbili zimekuwa zikitupiana tambo kuelekea mechi hiyo itakayopigwa leo majira ya saa 1 za usiku.
Mabosi wa timu zote mbili wamekuwa wakitamba kuwa kila mmoja yuko bora huku Mbao wakiahidi kuimaliza Yanga ili kuwafariji watani zao ambao ni Simba.
Post a Comment
0 Comments