MCHEZAJI SIMBA AKOSHWA BALAA NA KOCHA WA YANGA


Mkongwe na Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, King Kibadeni, amesifia mbinu ambazo alizitumia Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera katika mechi iliyowakutanisha watani hao wa jadi Septemba 30.

Kibadeni ameeleza kuwa mbinu na mfumo alioutumia Zahera kweli alifanikiwa kwa kwenda suluhu tasa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Mkongwe huyo ambaye aliwahi kufunga mabao matatu pekee 'Hat Trick' katika mechi iliyokutanisha timu hizo miaka ya nyuma, amempongeza Zahera kwa lengo lake kufanikiwa.

Licha ya kipa Beno Kakolanya kufanikiwa kuokoa kwa jitihada zote mashabulizi kutoka kwa straika hatari wa Simba, Kibadeni anaamini Zahera alikuwa na mchango wake.

Post a Comment

0 Comments