LIGI KUU VPL
SIMBA WAIVAA VIKALI YANGA
Yanga
waliitisha kikao na waandishi wa habari jana kunako makao makuu ya
klabu hiyo na kueleza kuwa walisitishwa na kitendo cha kiungo wa Simba,
James Kotei kumpiga beki wao Gadiel Michael.
Baada
ya tukio hilo, Yanga waliamua kukaa chini na kufikia maamuzi ya
kupeleka malalamiko TFF ili Kotei aweze kuadhibiwa kutokana na kucheza
mchezo usio wa kiungwana.
Licha
ya Yanga kufanya maamuzi hayo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara,
ameibuka na kulipua bomu kwa kueleza kuwa hata wao waliona alichofanyiwa
mchezaji wao lakini waliamua kukaa kimya.
Manara ameeleza kuwa katika mechi hiyo, beki wao Dante alimtishia kumpiga kichwa Hussein lakini waliamua tu kukaa kimya.
Ofisa
huyo mwenye maneno mengi amesema ifikie hatua wachezaji wote si Simba
wala Yanga waache kuonesha vitendo ambavyo si vya kiungwana ili
kutokuharibu taswira ya mchezo wa soka.
Post a Comment
0 Comments