Zahera arudi Congo, Yanga kuivaa Mbao bila Kocha



Yanga itamkosa kocha wake Mwinyi Zahera wakati ikishuka uwanjani kuwavaa Mbao FC wikiendi hii. 

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema Zahera hatakuwepo nchini kwa kuwa ataungana na timu ya taifa lake ya DR Congo itakayokuwa ikipambana kuwania kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika. 

"Kwa hiyo kocha hatutakuwa naye, lakini kila kitu kipo katika mpangilio na vijana wako tayari kwa kuwa wamekuwa na kocha muda wote," alisema. 

Zahera bado ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo na mmoja wa makocha wazalendo wa nchi hiyo wanaoaminika. 

Post a Comment

0 Comments