Ni Ancelloti na Klopp Ulaya leo, Vita ya wakubwa
Mabingwa mara tano wa Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, Liverpool ya nchini England watakua wageni wa Napoli katika mchezo wa kundi C utakaopigwa kwenye dimba la Stadio San Paolo nchini Italia usiku wa leo.
Liverpool iliyo chini ya Kocha wake Jurgen Klopp inaingia kwenye mchezo huo ikiwa vinara wa kundi hili wakiwa kileleni na pointi tatu wakifuatiwa na Napoli wenye alama moja sawa na Crvena Zvezda huku wababe wa Ufaransa, PSG wakishika mkia na alama sifuri.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na uimara wa vikosi hivyo ambapo Napoli chini ya mzoefu Carlo Ancellot inategemea wakali kama nahodha Marek Hamsik, Martens na Paolo Insigne huku Liverpool ikijivunia safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Mohammed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino.
Mchezo mwingine utaishuhudia PSG ikiikaribisha Zvezda katika dimba la Parc des Princess wakati Tottenham yake Mauricio Pochettino ikiikaribisha Barcelona.
Post a Comment
0 Comments