MKATABA WA YANGA NA KAMPUNI YA MACRON CHALIII, UONGOZI WATOA CHANZO CHA ANGUKO LAKE
Ule mkataba kati ya Yanga na kampuni ya vifaa vya michezo ya Macron, umeota mbawa.
Yanga waliingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni hiyo ambao ulielezwa utakuwa na thamani ya Sh bilioni tatu na ulisainiwa klabu hapo mbele ya waandishi wa habari.
Klabu ya Yanga, imethibitisha kuvunjika kwa mkataba huo ikieleza kwamba Macron ndiyo chanzo.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema kwa kuwa Macron walishinda kutekeleza makubaliano karibu yote waliyoingia kupitia mkataba huo, basi umevunjika.
"Maana hata jezi utaona klabu kwa sasa inajinunulia., maana yake hakuna mkataba tena na Macron," alisema Tena.
Post a Comment
0 Comments