VIDEO: Maamuzi ya Magufuli yaiokoa Taifa Stars



Maamuzi ya Rais waa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kuinunua ndege kubwa ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 200 unaweza ukawa mwanzo mzuri kwa Taifa Stars kufanya vizuri katika michezo yake dhidi ya Cape Verde. Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, ametangaza timu hiyo kuwa itatumia usafiri wa ndege hiyo kwenda Cape Verde na kurudi ili kuwapunguzia uchovu wa safari wachezaji ambapo kwa ndege za kawaida hutumia safari ya zaidi ya masaa 24. 

Post a Comment

0 Comments