TETESI ZA SOKA
POGBA, SCHHOLES, MOURINHO: TETESI KUBWA MOTO ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO
Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, 25. (The Sun)
Kiungo wa kati zamani wa Manchester United Paul Scholes, 43, anasema ameshangazwa kuwa meneja Jose Mourinho hakufutwa baada ya kushindwa kwa mabo 3-1 na West Ham siku ya Jumamosi. (BT Sport)
Mshambuliaji Mfaransa Christophe Dugarry anasema kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 46, mchezaji mwenzake wa zamani wa kimataifa hawezi kuchukua mahala pake Mourinho huko Old Trafford. (RMC Sport - kwa Kifaransa)
Mshambuliajia wa Arsenal Danny Welbeck anatarajiwa kumfuata kiungo wa kati Aaron Ramsey kuondoka Arsenal msimu ujao.
Mchezaji huyo mwenye miaka 27 wa kimataifa wa England yuko katika mwaka wake wa mwisho na hakuna makubaliano kuhusu mkataba wake mpya. (Mirror)
Manchester City wamekuwa wakimtazama kiungo wa wkati wa timu ya vijana ya Hoffenheim, Ilay Elmkies. MuIsrael huyo, 18, alifunga dhidi ya timu ya vijana wa Man City wikendi iliyopita. (Bild - in German)
Tottenham wako tayari kutoa ofa kwa mchezaji wa Paris St-Germain Adrien Rabiot mwezi Januari. Kiungo huyo wa kati mwenye miaka 23 raia wa Ufaransa hana mkataba msimu ujao na hivyo anaweza kuongea na klabu nyingine mwezi Januari. (Mirror)
Kocha wa muda wa Argentina Lionel Scaloni anasema hajazungumza na mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero kuhusu kurudi kwenye timu ya taifa. Aguero, 30, hakucheza katika mechi za kirafiki za kufuzu kwa kombe la dunia. (ESPN)
Chelsea watampa kiungo wa kati Mbrazil David Luiz mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Mkata wa mchezaji huyo mwenye miaka 31 unakamilika mwisho wa msimu. (Evening Standard)
Kutoka BBC
Post a Comment
0 Comments