SALAMBA AJA NA STAILI HII MPYA


Na George Mganga

Straika mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Lipuli FC baada ya msimu uliopita kumalizika, amekuja na staili mpya ya nywele.

Salamba ambaye bado hajapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwa mechi za ligi msimu huu ameamua kuzinyoa nywele zake na kutengeneza staili ya kiduku.



Mpaka sasa nyota huyo hajafanikiwa kucheka na nyavu ndani ya kikosi hicho na pengine anaweza akafungua ukurasa wa mabao leo Uwanja wa Taifa.

Simba itakuwa na kibarua leo dhidi ya African Lyon ambapo mechi hiyo itaanza majira ya saa 1 za usiku.

Post a Comment

0 Comments