WACHEZAJI SIMBA WAONDOLEWA STARS


Wachezaji wanne wa kikosi cha Simba waliokuwa wameitwa kwenye kambi ya Taifa Stars, wamerejeshwa katika klabu yao kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya African Lyon.

Simba watakuwa wanacheza na Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo kipute kitaanza majiya ya saa 1 kamili za usiku.

Aishi Manula, Shomari Kapombe, John Bocco na Jonas Mkude ndiyo wachezaji wa Simba waliokuwa wameitwa kambini Stars kwa ajili ya kujifua kujiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.

Cape Verde watakuwa wanaialika Stars nchini kwao, ambapo mechi hiyo ya kundi L itapigwa Oktoba 12 2018.

Aidha, wachezaji wengine waliorejea kwenye klabu zao ni wale wa Mtibwa Sugar ambao wataitumikia timu yao inayoshuka dimbani kucheza na KMC ya Kinondoni huko Manungu, Morogoro.

Post a Comment

0 Comments