LIGI KUU VPL
YANGA WAWATAHADHARISHA WABABE WA SIMBA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Yanga umeitahadharisha Mbao FC kuwa hawajaja Dar es Salaam kucheza na SImba.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, akiwataka Mbao kujipanga vilivyo kwani wamedhamiria kutoa maangamizi.
Nyika ameeleza kuwa Mbao wanajiamini wakijua kuwa wamekuja kucheza na Simba kitu ambacho haitakuwa rahisi kwao kupata matokeo.
Mwenyekiti huyo ambaye pia yupo kwenye kitengo cha Kamati ya Mashindano amefunguka hayo baada ya Mbao hivi karibuni kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi Simba huko CCM Kirumba, Mwanza.
"Awamu hii wanaenda kucheza na Yanga na siyo Simba, hivyo wanapaswa kujipanga kwa maana tumedhamiria kuchukua alama tatu" alisema Nyika.
Yanga itakuwa inawaalika Mbao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho Jumapili, mechi ikianza majira ya saa moja za usiku
Post a Comment
0 Comments