MICHEZO
UCHAGUZI MKUU SIMBA WAPIGWA KALENDA
Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kusogeza mbele siku yake uchaguzi wake mkuu kwa ajili ya kuwapata viongozi wake wapya watakaotawala kwa muda wa miaka minnne.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lihamwike, ameeleza uchaguzi huo sasa utafanyika terehe 4 Novemba badala ya 3 mwaka huu.
Lihamwike amesema kuwa Novemba 3 Simba itakuwa inashuka dimbani kucheza na JKT Tanzania hivyo ni vema mashabiki wakapata nafasi ya kuipa sapoti timu.
Baada ya mechi hiyo, kesho zoezi la uchaguzi litafanyika rasmi ili kuwachagua viongozi wapya ambao watakuwa madarakani kwa muda wa miaka minne mingine.
Wakati huo kikosi cha Simba kinashuka dimbani leo uwanja wa taifa kwa ajili ya mechi fhifi ya African Lyon itakayoanza majira ya saa 1 za usiku.
Post a Comment
0 Comments