MICHEZO
WAZIRI MWAKYEMBE AZITAJA GHARAMA ZA HOTEL HUKO CAPE VERDE
Na George Mganga
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amefunguka na kuelezea juu ya gharama za hoteli huko Cape Verde ambapo timu ya taifa 'Taifa Stars' itasafiri kucheza na wenyeji kuwania fainali za AFCON 2019.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya wadau ambao wameonesha nia ya kusafiri na timu kutaka kujua mapema gharama zitakuwaje ili waweze kujipanga.
Mwakyembe amesema tayari wameshatuma mtu ambaye ataenda kufuatilia hoteli hizo ambazo zitakuwa na gharama nafuu zitakazoweza kumudu mashabiki ambao watasafiri.
Waziri huyo anaamini watu watajitokeza kwa wingi kuungana na Stars ili kuipa hamasa kwenye mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na watanzania wengi.
Aidha, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limezidi kuwataka wadau kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za ndege ili wakaipe hamasa timu ya taifa
Post a Comment
0 Comments