YANGA YAMKANA OBREY CHIRWA, KISA HIKI HAPA




Chirwa ambaye aliichezea Yanga misimu miwili mfululizo, aliondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita akijiunga na klabu na Nagoon ya nchini Misri. 
Akizungumza na www.eatv.tv , kocha Mwinyi Zahera amesema, "Taarifa hizo ni za uongo, Chirwa alitupatia matatizo sana wakati Yanga ilikuwa na uhitaji wake".
"Yeye aliiacha timu ina matatizo mengi, karibia mechi nne au tano alikataa kucheza kwasababu hawakumlipa mshahara na pia alitakataa kufanya mazoezi kwasababu ya pesa. Tulisafiri kwenda Morogoro na wachezaji wachache sana, yeye alikataa kusafiri na timu, mchezaji wa vile siwezi kumrudisha kwenye timu yangu", ameongeza Mwinyi Zahera.
Chirwa alionekana katika mchezo wa Yanga wa wikiendi iliyopita, mchezo  ambao timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Alliance katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments