MICHEZO KIMATAIFA
Sakata la Mo Dewji lamuibua Gwajima
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kuliombea taifa kwani ndio wajibu wa kanisa na wawe mstari wa mbele katika kukemea mambo yasiyompendeza Mungu.
Gwajima amefunguka hayo jana wakati akihubiri katika ibada ya Jumapili Oktoba 21 kanisani kwake jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa ni wiki moja tangu kufanyika kwa maombi ya viongozi wakuu wa taifa pamoja na mfanyabishara aliyekuwa ametekwa Mohammed Dewji, ambapo Mungu amejibu na amepatikana.
Gwajima amesema kuwa waumini hawatakiwi kuegemea upande wowote linapokuja suala la kuliombea taifa dhidi ya vitendo viovu, ambavyo vinafanywa na watu wasio na mapenzi mema na kuwataka kuwa waaminifu na wazalendo.
"Wiki iliyopita tumefanya maombi kwa Mhe. Rais Magufuli, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wabunge na viongozi wa Kamati za Bunge, pamoja na mfanyabishara Mo Dewji, na leo tumekutana tena akiwa amepatikana ni jambo la kushukuru maana maombi yetu yamejibiwa", amesema Gwajima.
Mfanyabishara Mohammed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Oktoba 11, wakati akiwa mazoezini Collesium hotel na baadae Oktoba 20 alipatikana akiwa ametelekezwa katika viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam.
Post a Comment
0 Comments