HISTORIA YA SIR ANDY CHANDE
SIR ANDY CHANDY |
CHAPTER 1:BUKENE HOMETOWN AND CHILDHOOD.
Sir Andy Chande alizaliwa Mombasa Kenya 7th May 1928,lakini wazazi wake walikua wakiishi Tabora kijiji cha Bukene.baada ya mama yake kupata ujauzito alisafiri kwenda kujifungulia Mombasa.lakini licha ya kujifungua tarehe hiyo hakuandikishwa mpaka ilipopita miaka kadhaa baadae ambapo pia cheti chake cha kuzaliwa kiliandikwa tarehe nyingine kufuata kalenda ya kihindu ambapo aliandikwa kazaliwa 27th August 1929.hivyo kumfanya kua na birthday 2 tofauti(pia Malkia Elizabeth ana birthday 2 tofauti).
Baada ya mama yake kumzaa alirejea Bukene kijiji kilichokuepo kilomita 60 kutoka Tabora mjini.huko ndiko alipokulia Sir Andy Chande.alipofika kwa tamaduni za kihindu shangazi yake ndio alitakiwa kutoa jina na akambatiza Jayantilal kua jina lake(Andy Chande ni kifupi tu).
Baba yake Sir Andy alizaliwa India katika jimbo la Gujarat.Na mnamo wa mwishon mwa miaka ya 1919 alipande meli kuja kutafuta maisha Afrika na kufikia Mombasa,ambapo alipata ajira kwa mhindi mwenzake na alifanya kazi kwa uaminifu mkubwa.lakini baadae aliumwa macho akaamua kurudi India kutibiwa.huko alitamani kurudi Afrika na wakati huu alikuja mpaka Dar es Salaam.
Sir Andy Chande alipofika miaka 7(Mombasa alikua ana miaka 6 lakini lol)akaanza shule ambapo ilikua ya darasa moja ya wahindi watupu na lugha ya kufundishia ilikua ya kikwao ambapo watoto wengine wakihindi walikua wanasoma hapo hapo Bukene.kufikia mwaka 1935 biashara za baba yake zilikua zimeanza kutanuka na alihamia Tabora mjini na yeye Sir Andy Chande alikua kishamaliza elimu ya msingi.
Alipofika Dar baba yake Sir Chande alikuta reli ya kati inafanya kazi na wafanyabiashara wengi walikua wanaitumia kwenda huko mikoani kufanya biashara,na yeye akajitosa na hatimaye akafika kijiji cha Bukene ambapo kulikua kumechangamka kwasababu kulikua na kituo cha treni inasimama.baba yake Sir Andy Chande akaamua kusettle hapo na kuanza maisha miaka ya 1920's(yaani miaka hiyo mtu anatoka India anakuja bongo anaenda Tabora kusaka maisha,wewe ukiambiwa toka mjini uende Mtwara leo hautoki eti kijijini). Itaenndelea...
Post a Comment
0 Comments