Muendelezo wa historia ya Sir Jayantilal Keshavji Chandy (Sir Andy) - 1928 - 2017 sehemu 2



Ndivyo familia ya Sir Andy Chande ilivyojikuta inaishi Bukene ambapo mzee yule alifungua duka na baadae akaanzisha machine ya kusaga unga,kukoboa mpungu etc ambapo alikua anauza Tabora mjini na Dar es salaam.na baadae baba yake Sir Andy Chande aliwaalika ndugu zake kutoka India waje kushirikiana biashara walikuja wawili.

CHAPTER 2:SCHOOLDAYS


Sir Andy Chande alihamia Tabora mjini kuishi na baba yake aliyehamia Tabora mjini na biashara zake,na baba yake alikua akienda na kurudi Tabora-Bukene kuangalia familia,huku akimuacha Sir Andy Chande akikaa na baba mdogo.pale Tabora alianza sekondari,na anasema kwa mara kwanza ndio akaanza kushuhudia madhara ya ukoloni na haswa ubaguzi wake.

Anasema pale Tabora mjini alikuta watu wakiishi kwenye matabaka matatu ambapo kulikua na watawala wakoloni ambao ni wazungu na kulikua na tabaka la waAsia ambao ni wahindi na waarabu ambao wao walikua wafanyabiashara zaidi na weusi wakiwa vibarua na wakulima huku wao wazungu wakiwa watawala tu.

Anasema wazungu watoto wao walikua wakisoma kwenye shule nzuri za kiingereza,wahindi wao walisoma kwenye shule zao za kihindi na walifundishwa kwa kihindi huku weusi nao walikua na shule zao zilizofundisha kiswahili.

Siku moja alipotoka shuleni alipewa taarifa kua huko kijijini kwao Bukene,mama yake aliugua ghafla na akafariki maana hospital ilikua mbali karibu kilomita 22 kutoka kijiji Bukene.hali hiyo anasema ilimuumiza sana.

Baada ya mazishi ya mama yake familia iliamua ili kumsaidia baba yake Sir Andy Chande kulea watoto 9 alioachiwa na mkewe watoto wale watawanywe kwa ndugu mbalimbali.yeye Andy Chande alipelekwa Dar es Salaam kwa mjomba wake mmoja na akafikia maeneo ya barabara ya Morogoro(nahisi maeneo ya Kisutu au Fire).

Anasema alipofika Dar es salaam alijiunga na sekondari ya kihindi ambayo sasa hivi inafahamika kama Tambaza secondary.anasema huku Dar ndio akatoa ushamba kidogo akawajua wasichana na kwa mara ya kwanza akaonja bia  anasema shuleni hakua anafanya vizuri sana japo hakua wa mwisho,kwa kifupi anasema alikua mwanafunzi bora katika wale vilaza.

Anasema pia kua mbali na shule alikua akisaidia biashara pale nyumbani kwa mjomba wake,na ilimsaidia kuanza kujua na kujifunza biashara.lakini baadae baba yake akaamua kumwambia akasome masomo ya kidato cha 5&6 huko India baada ya yeye kumaliza kidato cha 4.

Sir Andy Chande akakubali na akapanda meli kwenda India.huko alifika jiji la Mumbai,enzi hizo likiitwa Bombay.huko alijiunga na shule moja iliyokua na wanafunzi mchanganyiko.wazungu,wahindi waliokua wametoka familia tajiri ndio waliopata fursa ya kusoma hapo na yeye akabahatika.

Anasema shule ile ilimjengea kupata marafiki ambao walikua wana connection duniani kote,maana walikua wanatoka kwenye familia za kitajiri.anasema kuna mwanafunzi mmoja ambae hata chakula chake(shule ilikua ya boarding)kilikua kinatoka mji mwingine.

Sir Andy Chande alifanikiwa kumaliza shule na kufaulu kawaida tu na baadae alijunga na chuo kikuu huko huko India kusomea degree ya historia.shule ile aliyosoma ya sekondari anasema alirudi baadae miaka 50 baada ya kumaliza akiwa na wanafunzi wenzake 1500 na walimu wastaafu wote kukutana kama kumbukumbu za shule hiyo wote wakiwa wametoka sehemu mbali mbali duniani.

Lakini anasema akiwa chuoni mwaka wa pili,baba yake alimpigia simu na kumwambia biashara zimetanuka sana na angependa sir Andy Chande akatishe masomo na arudi Tanganyika amsaidie biashara maana sasa walikua wamehamia DSM na wamefungua kiwanda kikubwa cha usagaji mahindi kwa gharama ya millioni 6 enzi hizo.sir Andy Chande kwa shingo upande akakubali kukatisha masomo yake na February mwaka 1950 akapanda meli na kurudi Tanganyika kuanza biashara. 
itaendelea...

Post a Comment

0 Comments