SEHEMU 5: HISTORIA SIR ANDY CHANDE

TANGANYIKA SOVEREIGNTY.


Kufikia mwishoni mwa miaka ya 1950 vuguvugu la kutaka Uhuru lilikua limepamba moto.mwaka 1958 serikali ya kikoloni ilitangaza kuitisha uchaguzi ambapo viti 30 vya ubunge vingegombewa,lakini kwa mgawanyo wa rangi.

Kila tabaka likitengewa siti 10 kila mmoja.weusi 10,wahindi 10 na wazungu 10.chama cha TANU kiligomea uchaguzi wakisema kua hata kama watapata siti zao 10 bado watazidiwa na wazungu na wahindi kwa pamoja na siti zao 20!.

TANU kulijaa wafahidhina ambao walikua na chuki wa wazungu na wahindi na walihamasisha kuwatenga watu wote weupe kwenye masuala ya kisiasa na wakipinga wasikaribishwe TANU.

Sir Andy Chande anasema Nyerere ndipo alipojitokeza kuanza urafiki na watu weupe na kuweka msimamo wa wastani na kuanza kuwaondoa hofu watu weupe.

Sir Andy Chande anasema kua Nyerere aliwashawishi sana wenzie wakubali kushiriki uchaguzi na mjadala uliodumu kwa siku 4 ukakubali kushiriki uchaguzi huku wale waliokua wakiwapinga watu weupe wakijitoa na kuunda chama chao kikiitwa ANC wakiongozwa na Zuberi Mtemvu.

Uchaguzi ulipofika TANU walishiriki na kushinda kwa kishindo siti zote 10 pia wale wagombea weupe waliowaunga mkono walishinda kwa kishindo akiwema Jamal(aliyekuja kua waziri wa fedha na Bryson mzungu aliyekuja  kua waziri wa afya.

Baada ya ushindi ule wazungu na wahindi wakamuamini zaidi Nyerere na serikali ya kikoloni ikarekebisha katiba kuruhus uchaguzi mwingine mwaka 1960 ambapo chama cha TANU kilishinda 67% ya siti zote na kufanikiwa kuunda serikali na Nyerere akiwa Waziri mkuu wa kwanza,pia serikali ya kikoloni ikiweka mipango ya kuikabidhi nchi kwa wazawa.

Sir Andy Chande anasema Oscar Kambona aliyekua katibu wa chama alimfuata na kumwambia Nyerere anataka yeye Andy agombee ubunge Tabora kwa tiketi ya TANU.yeye alikataa kwa kutotaka kuchanganya siasa na biashara,kitendo ambacho Nyerere kilimkera na baadae alikuja kumwambia wazi Sir Andy Chande.

Hatimaye mwaka 1961 mwezi December Tanganyika ikapata uhuru wake.
itaendelea...

Post a Comment

0 Comments