sehemu 7 :SIR ANDY CHANDE

NYERERE AND UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.

 


Baada ya Uhuru Tanganyika ikaanza safari ya kujitawala.Sir Andy anasema bado fukuto la kutaka watu weupe watengwe liliendelea na ikatoka presha kubwa kulazimisha wafanyakazi wa kizungu na wahindi kuachishwa kazi na nafasi zao kupewa weusi.mpango huo Nyerere aliukataa sanaa mpaka kufikia kujiuzulu kwa muda Uwaziri mkuu na kumuachia Kawawa na yeye kuanza kuzunguka nchi kuwaelewesha wananchi.

Mwaka 1963 mwisoni kulitokea jaribio la mapinduzi ya kijeshi yakilenga kumtoa Mwalimu madarakani ambapo Mwalimu ilimbidi kuita jeshi la Uingereza na Nigeria kutoa msaada ndipo uasi huo ulizimwa!.

Mwaka 1964 Tanganyika iliungana na Zanzibar kuunda Tanzania na Mwalimu Nyerere akawa Rais wa kwanza.Mwalimu Nyerere alimteua Sir Andy Chande kwenye maeneo mbali mbali kutumikia nchi haswa kwenye bodi za mashirika.

Bodi ya kwanza ilikua ya museum.Sir Andy Chande akapewa jukumu la kwanza kwenda kuongea na mgunduzi Dr.Leakey arudishe fuvu la zinjathropus TZ.Leaker alitoa masharti kadhaa ambayo yalihitaji fedha.

Sir Andy akamwambia waziri ambae alimjibu kua hakuna fedha za kuratibu urudishwaji wa fuvu hilo,Andy akaenda kwa Rais Nyerere ambae nae alimwambia serikali haina fedha katafute pesa unapopajua.Sir. Andy kwa msaada makampuni kama Unilever na ubalozi wa Denmark walisaidia fuvu lile kuja TZ na kuwekwa makumbusho ya taifa.


Sir Andy pia aliendelea na harakati zingine za kujenga nchi huku akiendelea na biashara zake.akiwa mwenyekiti wa bodi ya elimu ya mkoa,Sir Andy Chande alifanikisha ujenzi wa shule ya viziwi na watu wenye ulemavu jijini Dar es salaam eneo la Buguruni,pia walijenga shule ya sekondari ya Shaaban Robert.pia kuchangia ujenzi mbali mbali wa shule zingine.

Kutokana na michango yake Meya wa zamani wa DSM Kitwana Kondo alimfuata na kumwambia anataka mtaa mmoja upewe jina lake,lakini alikataa kwa kusema wasubiri akifa ndio watoe jina lake kwa mtaa.


sir Andy Chande anasema baada ya Tz kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Uingereza na wao kukata msaada.uchumi ulianza kuyumba na akaanza kusikia fununu serikali inataka kutaifisha baadhi ya sekta kuu za uchumi.

Sir Andy Chande mbali ya kua mfanyabiashara serikali ilipenda sana kumtumia kwenye mambo yake.ambapo aliteuliwa kua mwenyekiti wa bodi ya Air Tanzania,Bandari pia mshauri wa kwenye suala la ujenzi wa wa reli ya TAZARA.

Sir Andy anasema serikali ya Tanzania ilipotaka kuanzisha uhusiano wa kibiashara na kitamaduni na serikali ya Misri yeye,waziri mmoja na katibu mmoja waliteuliwa kuongoza ujumbe kwenda Misri kwa mazungumzo.

Anasema wakiwa kwenye ndege kwenda Misri walikunywa sana pombe na wakafika Misri 'wamependeza' kidogo.lakini anasema baada ya kufika hotelini kama saa mbili usiku,waziri wa utamaduni wa Misri aliwaambia watoke out kwenda night club moja.anasema walizidi kulewa na kurudi hotelini alfajri wakitambaa.


Lakini kesho yake saa tatu asubuhi wakaamka na yule waziri aliyekua kalewa sana bado alionekana pombe ziko kichwani na uso wa kilevi alivaa miwani wakaenda kwenye mkutano ambapo Sir Andy Chande anasema waziri yule alitoa hotuba moja nzuri sanaaaaa utafikiri sio yeye aliyekua kalewa chakari masaa machache yaliyopita.

itaendelea...

Post a Comment

0 Comments