SEHEMU 8:ANDY WINES AND BREAD AND BOXES.





Sir Andy akaanza kazi kama mtendaji mkuu muajiriwa wa kampuni iliyokua yake mwenyewe kabla serikali kuitafisha na kuimiliki.lakini baadae serikali ikaamua viwanda vyote vilivyobinafisishwa viwe ndani ya shirika moja na Sir Andy Chande akawekwa kama mkurugenzi mkuu.

Shirika hili lilikua chini ya wizara ya kilimo.waziri wa kilimo wakati huo aitwae bryceson mzungu pekee katika baraza la mawaziri na alikua rafiki wa karibu wa Nyerere pia jirani yake pale Msasani alipokua anaishi,nyumba ya jirani.

Anasema yeye na huyu waziri hawakupatana kwasababu alikua anaingilia sana utendaji wake na hakua anafahamu vyema biashara yenyewe.

Sir Andy akiwa ndio mkurugenzi wa NMC,anasema mwanzo kabisa alipishana na waziri baada ya waziri kumwambia awafukuze kazi wafanyakazi wake watatu kwasababu anazozijua yeye waziri.Sir Andy aligoma katakata akisema wafanyakazi wake hawana makosa na hakuna ushahidi,huku waziri akisisitiza watimuliwe.

Lakini Sir Andy alikomaa na mgogoro ukawa mkubwa mpaka kuitishwa kikao cha bodi.baada ya uchunguzi na vikao kadhaa ikaja kugundulika kumbe wale wafanyakazi walisingiziwa kwa husda za watu na kama sio Andy kuwatetea mpaka kuweka kibarua chake mashakani wangekua long time kitambo hawana ajira.


Sir Andy anasema japo biashara yake ilikua ni ya usagaji wa nafaka.alishangaa baada ya waziri wa kilimo wakati akiwa bado Bryceson alipompa taarifa kua serikali imedhamiria kuanza kutengeneza mvinyo(wine).

Yeye Sir Andy anasema alikua hajui chochote kuhusu wine na alishangaa na kuomba asipewe jukumu hilo la kusimamia kiwanda cha wine.lakini waziri kama kawaida yake akamwambia hilo lako kama hautaki kamwambie Rais.



Sir Andy akaenda mpaka Dodoma kuona zabibu zinapolimwa gereza la Isunga.tatizo likaja kua Tanzania haina utaalamu wala watu wenye ujuzi wa kutengeneza wine!.

Sir Andy anasema ikambidi kwenda kwa balozi wa ufaransa nchini kuomba msaada jinsi watakavyoweza uzalishaji.anasema balozi yule alishangaa sana na alishtuka sana kwa wakati ule kusikia TZ inataka kutengeneza wine na baada ya kumsikiliza hakua na msaada wowote.Sir Andy akamaliza chai yake akaondoka zake!.

Lakini hakukata tamaa akaenda kwa balozi wa Italia nchini.huyu alipenda wazo hili na akakubali kusaidia kwa kuleta mtaalamu kutoka kwao aje kutengeneza mvinyo hapo Dodoma.

Anasema baadae nae balozi wa Ufaransa alipotulia akakubali kutoa msaada wa mafunzo kwa watanzania wawili kupelekwa ufaransa kufunzwa mambo ya mvinyo.anasema hatimaye baada ya miezi kadhaa wakafanikiwa kuzalisha wine za mwanzo na wakafanya uzinduzi!.


Sir Andy anasema kupishana kauli tena na waziri kulikuja kwenye suala la bei za mchele.anasema yule waziri alikua anadhania kua biashara hizi wanatengeneza faida kubwa sana.

Kwasababu zake za kisiasa akatangaza kushushwa kwa bei ya mchele bila kushauriana na Sir Andy Chande.matokeo yake yakaibuka matatizo mawili.

Mosi demand ya mchele ikawa kubwa sana kuliko uzalishaji wa viwanda maana bei ilikua chee na kila anataka mchele sasa.

Pili bei iliyotangazwa na Waziri ilikua chini sana kiasi kwamba walikua wanauza kwa hasara badala ya faida.kwahiyo shirika likaanza kupata hasara.sir Andy alijaribu kuongea na waziri na kumuelewesha lakini alikua mbisha sana!.

Anasema aliomba kuonana na Rais mwenyewe lakini Rais Nyerere alikataa kuonana nae!.anasema akaendelea kuendesha shirika kwa hasara,lakini kwa bahati nzuri Mzungu yule alihamishwa pale na akateuliwa waziri mpya aitwae Joseph Mungai.

Sir Andy anasema Mungai kidogo alikua muelewa na walielewana na alimsaidia kumkutanisha na Nyerere na Sir Andy akamueleza ukweli wa mambo mheshimiwa Rais.Nyerere akaamuru Sir Andy aachiwe Uhuru wa kupanga bei anayotaka.


itaendelea...

Post a Comment

0 Comments