sehemu ya 4 SIR ANDY CHANDE

MARRIAGE: MY BEAUTIFUL JAYLI.

Alipofikisha miaka 25 Sir Andy Chande familia yake iliona sasa inafaa atafutiwe mke wa kuoa.kwanza baba yake na baba mdogo walisubiri kuona labda ana mchumba wake mwenyewe,ila hawakuona kitu japo sir Andy Chande mwenyewe anasema alikua ana wapenzi kadhaa na alikua anasafiri weekend mara kwa mara kwenda Zanzibar kwenye starehe.pia alipenda sana kutoka na marafiki kwenda kunywa pombe inshort alikua bado anapenda maisha ya ujana.

Familia yake ikampa taarifa kua sasa lazima aoea na wamemtafutia mchumba.mchumba mwenyewe alipatikana huko Kenya katika mji wa Kisumu.lakini kabla hawajaanza taratibu za ndoa mchumba yule siku moja akivuka na gari kwenye mto ambapo kulikua na mafuriko,alisombwa na kupoteza maisha!.

Baadae familia yake ilihamia nchini Uganda kusaka mchumba na moja kwa moja walienda kwa familia ya Madhvani,ambao ilikua familia ya kitajiri sana Uganda na pengine familia ya kihindi tajiri zaidi Afrika mashariki kwa wakati huo.

Wazazi wa pande zote 2 walikubaliana na Sir Andy Chande akaambiwa asafiri hadi Jinja Uganda kwenda kumuona mchumba kwenye familia hiyo ya kitajiri binti wa miaka 16 aitwae Jayli.

Sir Andy anasema alipofika Uganda kumuona mchumba aliingia uoga sana maana familia ile ilikua matajiri mno ambapo walikua wakimiliki mashamba makubwa ya miwa yanafokia ekari 20,000!(ndio ekari elfu shirini)wakizalisha sukari!.pia binti mwenyewe mdogo alikua tayari anaendesha gari lake mwenyewe.hiyo ilimfanya Andy awe mpole kidogo.

Lakini familia ile ilimkubali na mipango ya ndoa ikaanza.japo ndoa iliahirishwa mara 2 kwa misiba iliyotokea kwenye familia zote 2,mpaka ilipofika mwaka 1954 ndio waliweza kuoana.

Harusi ilifanyika Jinja Uganda.familia ya kina Sir Andy ilikodisha ndege ya shirika la East African airways yenye kubeba watu 28 wakapanda ndugu hadi Uganda ambapo walikuta harusi ya kishindo imeandaliwa.

Baada ya harusi walirudi Dar kuanza maisha ya ndoa nyumbani kwa baba yake Sir Andy Upanga.baadae mkewe alishika ujauzito na mwaka 1956 wakafanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume.
itaendelea

Post a Comment

0 Comments