TAHADHARI: UWEZEKANO WA KUTOKEA VIMBUNGA PACHA BAHARI YA HINDI

 TMA inatoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa vimbunga pacha magharibi mwa Bahari ya Hindi upande wa kaskazini na kusini mwa Ikweta na hivyo kuwa na uwezekano wa kuathiri mifumo ya hali ya hewa nchini

 Migandamizo hiyo midogo pacha inaelekea kuimarika na kuwa vimbunga katika Pwani ya Somalia (Upande wa Kaskazini mwa Ikweta ) na Kaskazini Mashariki mwa Kisiwa cha Madagascar (Kusini mwa Ikweta)

 Aidha, mgandamizo mdogo wa hewa uliopo kusini magharibi mwa bahari ya Hindi (karibu na kisiwa cha Madagascar) unatarajiwa kuimarika na kuelekea kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar, na hivyo unatarajiwa kusababisha ongezeko la mvua pamoja na vipindi vya mvua kubwa hususan katika baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini ya nchi yetu kati ya terehe 5 na 6 Disemba 2019

 Mamlaka imeendelea kutoa tahadhari ya vipindi vifupi vya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es salaam na Pwani na angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Ruvuma

 Kwa upande mwingine, mgandamizo mdogo wa hewa katika pwani ya Somalia unatarajiwa kuendelea kuwa mbali na pwani ya Tanzania na hautarajiwi kuwa na madhara katika nchi yetu.

chanzo :jamiiforum

Post a Comment

0 Comments