Aliyemkalisha Ajibu wa Yanga Atoa Ahadi kwa Taifa



NA ELBOGAST MYALUKO
Mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile ambaye leo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu soka Tanzania bara mwezi Septemba, amesema lengo lake si kuisaidia Mbeya City tu bali anajituma ili asaidie taifa.


Kushoto ni Ibrahim Ajibu na Eliud Ambokile

Katika kinyang'anyiro hicho Ambokile amewashinda  Ibrahim Ajibu wa Yanga na Stamili Mbonde wa Mtibwa Sugar.

''Nawashukuru wachezaji wenzangu wa Mbeya City bila wao nisingepata mafanikio haya, nachoweza kusema tu mpira ni kazi yangu na malengo yangu sio kuitumikia Mbeya City pekee bali napambana ili siku moja taifa langu lijivunie mimi'', amesema.

Ndani ya mwezi huo Ambokile alionesha uwezo mkubwa uwanjani ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne, ambapo mbeya City ilishinda michezo miwili sare 1 na kupoteza miwili.

Ambokile ambaye kwasasa ndiye kinara wa mabao kwenye ligi kuu soka Tanzania bara akiwa amefunga mabao 6 kwenye mechi 10, atakabidhiwa zawadi ya tuzo pamoja na shilingi milioni moja.

Post a Comment

0 Comments