MICHEZO KIMATAIFA
Ronaldo, majanga kama Messi tuu
Nyota wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo
ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza michezo miwili
ijayo ya michuano ya ligi ya mataifa ya Ulaya.
Kocha
wa timu hiyo ya taifa, Fernando Santos amemwacha nyota huyo katika
ratiba ya mechi mbili zijazo, ambapo timu ya taifa ya Ureno itacheza na
Poland na Scotland kuanzia wiki mbiili zijazo.
Ripoti zinaeleza kuwa siku za karibuni, Ronaldo aliwasiliana na kocha, Santos pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo, Fernando Gomez akiwaomba kuwa asiitwe katika kikosi cha timu ya taifa hadi mwezi Novemba , japo haifahamiki kama ni sababu hiyo ndiyo iliyopelekea kutoitwa kwa wakati huu katika kikosi.
Siku za karibuni, nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi aliachwa katika kikosi cha Argentina kilichotangazwa kwaajili ya michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki ya mwezi huu. Ikiwa ni mara ya pili, baada ya kuachwa katika kikosi hicho kwenye michezo yake mwezi uliopita.
Ronaldo ambaye ameifungia mabao matatu klabu yake ya Juventus katika ligi kuu nchini Italia Serie A mpaka sasa, hajaichezea timu hiyo ya taifa tangu ilipoondolewa na Uruguay katika hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi mwezi Juni.
Aliachwa pia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Croatia ambao timu hizo zilitoka sare ya 1-1 pamoja na mchezo ambao Ureno ilishinda dhidi ya Italia kwa bao 1-0 mwezi uliopita ilia pate muda wa kuzoea mazingira ya klabu yake mpya ya Juventus.

Post a Comment
0 Comments