Azam Fc yatoa tahadhari kwa vilabu ligi kuu

Hii leo klabu ya Azam Fc inacheza mchezo wake wa saba wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Azam FC.
Azam FC yenye alama 12 inazisaka alama tatu katika mchezo huo ili iweze kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi, ikifikisha alama 15, nyuma ya kinara Mtibwa Sugar yenye alama 15 baada ya kushinda mchezo wake wa wiki hii.
Akizungumza kuelekea mchezo huo, Afisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd Maganga amesema,
" Wachezaji wote ni wazima na hatuna majeruhi, tayari Yakub Mohamed ameshaanza mazoezi pamoja na mwenzake Donald Ngoma ambaye alicheza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Lipuli japo wa dakika chache alipoingia kipindi cha pili ".
" Ngoma ameleta matumaini makubwa kwa kushirikiana na wenzake na ameonesha kuwa yeye ni mchezaji mkubwa, kwa dakikia chache alizocheza alipeleka misukosuko kwa mahasimu japokuwa hatukupata goli lakini sasa tumepata kifaa halisi kitakachotusaidia kupata ushindi katika michezo ijayo ya ligi kuu Tanzania bara ", ameongeza.
Azam FC ilimsajili Donald Ngoma msimu huu akitokea Yanga, siku chache baada ya kukamilisha usajili huo alipelekwa nchini Afrika Kusini kufanyiwa matibabu ya mguu wake ambao ulikuwa ukimsumbua tangu msimu uliopita akiwa na Yanga.

Post a Comment

0 Comments