RUVU SHOOTING YATOA KITISHO KWA TIMU LIGI KUU


Timu ya Ruvu Shooting “Timu ya Wananchi wa Pwani” ya mkoani hapa, leo ipo mkoani Kagera kucheza dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani humo.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa timu hiyo imefika salama mkoani humo, na akatamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Bwire ameongeza kuwa, walichofuata huko si kingine bali ni alama zote tatu na akawataka wenyeji wao kujiandaa na kichapo.

Amesema kuwa, kwa sasa timu yao ipo vizuri sana na inatembeza vipigo kokote kule iwe kwenye uwanja wa nyumbani ama wa ugenini.

“Tumefika salama huku Kagera na wachezaji wote wana ari kubwa ya ushindi na kutokana na ubora wa timu yetu, tuna uhakika wa ushindi,” alisema Bwire

Post a Comment

0 Comments