TETESI KUBWA NA KALI ZA MOTO KUHUSU SOKA BARANI ULAYA LEO IJUMAA OKTOBA 5 2018
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anaweza kufukuzwa mapema wiki ijayo kama timu yake itafungwa na Newcastle United siku ya Jumamosi. (Sun)
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino ndio anategemewa kuchukua nafasi ya kuwa kocha wa Manchester United kama Mourinho atafukuzwa. (Independent)
Mlinda mlango wa Manchester United David De Gea, kiungo wa kati Paul Pogba na mshambuliaji Anthony Martial walikuwa wanatahitajika na Zinedine Zidane wakati akiwa meneja wa Real Madrid. (Manchester Evening News)
Mlinzi wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger, 25, anaamini kwamba Eden Hazard ndio mchezaji mahiri zaidi katika timu ya Blues inayoongozwa na Maurizio Sarri. (Standard)
Mshambuliaji wa Manchester City Benjamin Mendy, 24,anasema mazoezi makali anayopewa na meneja Pep Guardiola yanamfanya kuwa bora zaidi. (Manchester Evening News)
City watatumia kamera ya kiwango cha juu ili kuwapeleleza wachezaji wake wakiwa katika basi katika mechi ya Jumapili watakayocheza na Liverpool baada ya gari walilopanda msimu uliopita kushambuliwa kwa mawe.(ESPN)
Wakati huo huo kiungo wa kati kinda wa City Phil Foden, 18 amenunua nyumba ya £ milioni 2 kwa ajili yake na familia yake kwa lengo la kuimarisha umoja wao licha ya umaarufu aliokuwa nao. (Mail)
Timu ya Arsenal inajaribu kumuwania meneja mkuu wa Jeventus, Giuseppe Marotta ambaye anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo lakini Inter Mian pia imeonyesha nia.
Meneja wa zamani wa England Fabio Capello amesema ameambiwa na meneja wa Manchester United Jose Mourinho kuwa alitaka kumsajili Milan Skriniar ,23, kutoka Inter Milan na Kalidou Koulibaly ,27,wa Napoli msimu uliopita. (Sky Italia via Football.London)
Mmiliki wa Newcastle,Mike Ashley amehaidi kuwapeleka wachezaji wake likizo kama hawatoshuka daraja EPL. (Mail)
Ashley anadaiwa kula tambi za £ 7.95 wakati akiwa katika kikao cha muda wa saa nne akiwa na meneja Rafa Benitez na wachezaji wiki hii. (Chronicle)
Mlinzi wa Sweden na Helsingborgs IF Andreas Granqvist, 33, anasema alikuwa anatania katika uvumi unaosambaa unaomuhusisha yeye na Manchester United. (FotbollDireckt via Manchester Evening News)
Kutoka BBC
Post a Comment
0 Comments