klabu ya Chelsea imekamata saini ya mshambuliaji wa borussia dortmund...








Klabu ya Uingereza, Chelsea imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Christian Pulisic kwa kitita cha Euro 64 Milioni, sawa na $73.1 Milioni.

Chelsea imekamilisha hatua hiyo lakini imewapa wapiga soka hao wa Bundesliga awachezee kwa mkopo katika kipindi cha msimu huu kabla hajahamia rasmi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao wa kiangazi.
Klabu hiyo ya Uingereza imemnasa mchezaji huyo machachari mwenye umri wa miaka 20 kabla ya kukamilisha hatma ya mkataba wake na Dortmund uliokuwa ukamilike mwaka 2020.
“Ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu wa Christian kucheza Ligi Kuu ya Uingereza. Hayo yalikuwa matakwa ya mchezaji huyu wa Marekani kwa muda mrefu, hivyo sisi hatukuweza kuongeza muda wa mkataba wake,” amesema Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Michael Zorc.
on Video: Mikopo elimu ya juu wabunge wachachamaa, Makinikia yaleta kiam




Post a Comment

0 Comments