MICHEZO
BREAKINGNEWS: SIMBA YAPATA PIGO
Ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu Simba icheze na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, kuna hatihati ya kiungo mnyumbulifu wa timu hiyo, Jonas Mkude kuukosa mchezo wa Taifa Stars na Cape Verde.
Taarifa ambazo mtandao huu umezinasa zinasema Mkude aliumia kwenye mechi hiyo ambayo Simba walifanikuwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Kuumia kwa mkude kunaweza leta pengo kwa Stars na hata Simba haswa kwenye nafasi ya kiungo kwa mechi zijazo kwani haijajulikana lini atarejea kuwa fiti.
Hata hivyo taarifa kutoka kwa Daktari wake, zinasema kiungo huyo hakuumia kiasi cha kwamba anaweza akakaa muda mrefu nje ya uwanja, hivyo subira inatakiwa kusubiria apone.
Mkude anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Stars kitakachoshuka dimbani Oktoba 12 kukipiga na Cape Verde kwa ajili ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019.
Post a Comment
0 Comments